Back

ⓘ Io, Mshtarii. Io ni mmoja wa miezi ya sayari Mshtarii. Kwa ukubwa ni mwezi wa tatu wa sayari hiyo na kipenyo chake ni km 3.642. Hii ni kubwa kidogo kuliko Mwezi ..
Io (Mshtarii)
                                     

ⓘ Io (Mshtarii)

Io ni mmoja wa miezi ya sayari Mshtarii. Kwa ukubwa ni mwezi wa tatu wa sayari hiyo na kipenyo chake ni km 3.642. Hii ni kubwa kidogo kuliko Mwezi wa Dunia yetu.

Io ilitambuliwa mwaka 1609/1610 na Simon Marius na Galileo Galilei wakati hao walipokuwa watu wa kwanza kutumia darubini kuangalia nyota wakaona miezi minne mikubwa zaidi ya Mshtarii. Marius alipendekeza majina ambayo yamepokewa hadi leo kwa miezi hiyo minne waliyoiona.

Tabia ya pekee ya Io ni idadi kubwa ya volkeno hai zilizotazamwa hadi sasa. Hakuna gimba jingine katika Mfumo wa Jua lenye idadi kubwa hivi.

Volkeno hizo zatoa mawingu makubwa ya sulfuri na dioksidi ya sulfuri yanayoenea hadi kimo cha km 500 juu ya uso wa Io. Mwezi huwa pia na milima mirefu, mingine inashinda kimo cha Mlima Everest, ambao ni mlima mrefu kabisa duniani.

Tabia za Io hazikujulikana kwa muda mrefu lakini vipimo na picha zilizopigwa na vipimaanga Voyager 1 na 2, baadaye na "Galileo" iliyopita karibu mara kadhaa, zilileta data kama hizo.

Sawa na mwezi wa Dunia, mzunguko wa Io kwenye mhimili wake unashikamana kabisa na muda wa obiti yake "tidally locked"; kwa hiyo ni upande uleule unaoangalia sayari yake.

Tofauti na miezi mingine katika Mfumo wa Jua, hakuna kasoko nyingi zinazoonekana; inaaminiwa kwamba vumbi kutoka volkeno linajaza kasoko zinazotokea baada ya kupigwa na asteroidi.

                                     
  • IO au io ni kifupi cha: Kodi ya ISO 639 - 1 ya lugha ya Kiido Kodi ya ISO 3166 - 1 ya nchi ya Eneo la Uingereza katika Bahari Hindi Io Mshtarii mwezi wa
  • Mshtarii pia Mshiteri, Mushtarii au Mshatira, kutokana na Kiarabu المشتري al - mshtari na hata Jupita kutokana na Kiingereza Jupiter ni sayari ya tano
  • inashikamana na obiti za miezi Europa na Io katika uhusiano wa 1: 2: 4. Ganimedi ni mmoja wa miezi ya Mshtarii iliyotambuliwa mnamo 7 Januari 1610 na Galileo
  • katika angahewa ya Mshtarii Jupiter jinsi ilivyoonekana kutoka Voyager 1. Picha ya Io mwezi wa Mshtarii Picha ya angahewa ya Mshtarii ilivyopigwa na Voyager
  • ya kufanyia utafiti sayari ya Mshtarii Jupiter na miezi yake. Iligundua sayari ya Jupita na mwezi wake. Ilifika Mshtarii mnamo 1995. Sehemu ya kwanza

Users also searched:

...