Back

ⓘ Jangwa la Kalahari. Kalahari ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi na nusu yabisi kusini mwa Afrika lenye kilomita za mraba 900.000 hivi katika Botswana na sehem ..
Jangwa la Kalahari
                                     

ⓘ Jangwa la Kalahari

Kalahari ni eneo kubwa lenye tabianchi yabisi na nusu yabisi kusini mwa Afrika lenye kilomita za mraba 900.000 hivi katika Botswana na sehemu za Namibia na Afrika Kusini.

Ni tofauti na jangwa la Namib lililopo nyuma ya pwani ya Atlantiki ya Namibia na Angola.

                                     

1. Jina

Jina "Kalahari" linatokana na neno la Kitswana "Kgala", linalomaanisha "kiu kubwa" au kutoka "Kgalagadi" inayomaanisha "pasipo maji". Kalahari ina maeneo makubwa yaliyofunikwa na mchanga tu bila maji ya kudumu.

                                     

2. Tabia

Kalahari huwa na wanyama na mimea kadhaa kwa sababu sehemu kubwa si jangwa kabisa. Kuna kiasi kidogo cha mvua. Majira ya joto ni makali sana. Maeneo yenye ukavu zaidi huwa na milimita 110-200 za mvua kwa mwaka. Maeneo yenye usimbishaji mkubwa zaidi huwa na milimita 500.

Makorongo makavu ya mito ya zamani yanapatikana kaskazini mwa Kalahari, yakijaa maji wakati wa mvua na yanayobaki kama mabwawa madogo kwa miezi kadhaa.

                                     

3. Beseni la Kalahari

Beseni la Kalahari ni pana zaidi likikusanya maji yote yanayotiririkia mle kwenye eneo la km 2 milioni 2.5. Beseni hilo huenea hadi Botswana, Namibia na Afrika Kusini, pamoja na sehemu za Angola, Zambia na Zimbabwe.

Kuna mto mmoja wa kudumu pekee ambao ni mto Okavango. Okavango inaishia katika delta ya ndani inayofanya sehemu za vinamasi vyenye wanyamapori wengi.

Sehemu kubwa ya jangwa nchini Botswana imekuwa sehemu ya Hifadhi ya Kalahari ya Kati.

                                     

4. Marejeo mengine

 • Main, Michael 1987. Kalahari: lifes variety in dune and delta. ISBN 1868120015.

Kigezo:Commons and category

 • Kalahari deserts forgotten influence on carbon levels
 • "Cry of the Kalahari"

Majiranukta kwenye ramani: 23°S 22°E

                                     
 • Hifadhi ya Kalahari ya Kati Central Kalahari Game Reserve ni mbuga kubwa ya wanyamapori katika jangwa la Kalahari la Botswana. Ilianzishwa mwaka 1961
 • Okavango unaokwisha katika jangwa la Kalahari huko Botswana. Delta hii ni eneo la mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa Mto wa Ewaso Nyiro katika
 • tangu miaka 1980 kwa ajili ya athari nzuri kwa afya. Asili yake ni Jangwa la Kalahari lakini siki hizi hukuzwa nchini Nyuzilandi, Australia, Chili, Italia
 • pamoja na Gobabis na Witvlei. Nossob na Eiseb ni mito muhimu zaidi. Gobabis Witvlei jangwa la Kalahari Wikimedia Commons ina media kuhusu: Mkoa wa Omaheke
 • katika milima ya Bié inapojulikana kwa jina la Kubango. Mwendo wake wa km 1600 ni kusini tu hadi jangwa la Kalahari unapoishia kwenye delta ya barani. Katika
 • 1600 km katika jangwa la Kalahari Botswana Mikono ya delta na maziwa yamejenga mazingira yenye mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa kubwa. Delta
 • unakwisha kwenye delta yake katika jangwa la Kalahari Botswana Delta hii ni eneo lenye mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa kubwa. Delta inavuta watalii
 • kati ya Botswana na Zambia kuvukia mto Zambezi. Jangwa la Kalahari linafunika theluthi mbili za eneo la Botswana. Moja ya maeneo muhimu nchini Botswana
 • Sehemu kubwa ya nchi ni kavu sana na jangwa za Namib na Kalahari zinafunika asilimia kubwa ya uso wa nchi. Jangwa la Namib liko upande wa magharibi likifuata
 • Mdogo Blue - black plated lizard Gerrhosaurus auritus, Guruguru wa Kalahari Kalahari plated lizard Gerrhosaurus bulsi, Guruguru wa Laurent Laurent s

Users also searched:

...
...
...