Back

ⓘ Jiografia ya Kenya inahusu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ni ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska 580.367 km 2 ikiwa na eneo la kilomita mraba ..
Jiografia ya Kenya
                                     

ⓘ Jiografia ya Kenya

Jiografia ya Kenya inahusu nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambayo ni ya 47 kwa ukubwa duniani ikifuata mara Madagaska 580.367 km 2 ikiwa na eneo la kilomita mraba 580.367.

Kutoka pwani ya Bahari ya Hindi, nyanda za chini zimeinuka hadi milima ya kati. Milima hii imetenganishwa na eneo la Bonde la Ufa; sehemu tambarare yenye rutuba upande wa mashariki. Milima ya Kenya ni kati ya zilizofaulu kwa kilimo barani Afrika.

Eneo hili la milima ndilo la juu zaidi nchini Kenya na la pili kwa urefu barani Afrika: Mlima Kenya, unaofikia urefu wa mita 5.199 futi 17.0570 5.199 m 17.057 ft na ni eneo lenye mito ya barafu. Ngambo ya mpaka wa Tanzania Mlima Kilimanjaro 5.895 m/19.341 ft huweza kuonekana upande wa kusini.

Kenya ni nchi yenye jua kali na nguo za majira ya joto huvaliwa mwaka mzima. Hata hivyo, huwa na baridi usiku na pia asubuhi na mapema.

Hali ya hewa ina joto na unyevu sehemu za pwani, joto kiasi sehemu za bara na ni kame katika sehemu za kaskazini na kaskazini-mashariki mwa nchi. Hata hivyo kuna mvua nyingi kati ya Machi na Aprili, na mvua ya kadiri kati ya Oktoba na Novemba. Halijoto huwa juu zaidi miezi hii yote.

Mvua ya masika hunyesha kuanzia Aprili hadi Juni. Mvua ya vuli nayo hunyesha kuanzia Oktoba hadi Desemba. Wakati mwingine mvua hii huwa nyingi na aghalabu hunyesha wakati wa alasiri na jioni. Majira ya joto jingi ni kuanzia Februari hadi Machi nayo ya baridi ni Julai hadi Agosti.

                                     
  • Webuye ni mji wa Kenya magharibi katika kaunti ya Bungoma. Wakazi upande wa Kenya walikuwa 65, 280 wakati wa sensa ya mwaka 2009. Sensa ya Kenya 2009 Archived
  • ndogo upande wa Kenya katika kaunti ya Marsabit. Wakazi upande wa Kenya walikuwa 37, 378 wakati wa sensa ya mwaka 2009. Sensa ya Kenya 2009 Archived Januari
  • Nanyuki ni mji mdogo katikati ya Kenya kaskazini - magharibi chini ya Mlima Kenya mwishoni kwa reli. Mstari wa ikweta unapita katika eneo la mji na Nanyuki
  • Limuru ni mji wa kaunti ya Kiambu, Kenya Wakati wa sensa ya mwaka 2009, mji ulikuwa na wakazi 104, 282. Sensa ya Kenya 2009 Archived Januari 9, 2019 at
  • Kiambu ni mji wa Kenya ya Kati, makao makuu ya kaunti ya Kiambu. Wakati wa sensa ya mwaka 2009 ulikuwa na wakazi 88, 869. Sensa ya Kenya 2009 Archived Januari
  • Ruiru ni mji wa Kaunti ya Kiambu, ipatikanayo katikati ya Kenya Mji huu uko katika umbali wa takribani kilomita 3 kutoka katika Mpaka wa Nairobi. Una
  • wa Kenya ya kati, takriban kilomita 100 kaskazini kwa Nairobi, miguuni mwa safu ya Aberdare ikitazama mlima Kenya Nyeri ni makao makuu ya Kaunti ya Nyeri
  • Kaunti ya Nyeri ni mojawapo ya kaunti za Kenya zilizopo baada ya katiba mpya ya Jamhuri ya Kenya kupatikana mwaka 2010. Makao makuu yako Nyeri. Kaunti ya Nyeri

Users also searched:

mkuu wa mkoa wa mara anaitwa nani, tuki,

...
...
...